Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulio ya walinzi amani Usomali yalaaniwa na KM

Mashambulio ya walinzi amani Usomali yalaaniwa na KM

Kadhalika KM kwenye risala yake ya ufunguzi wa mahojiano na waandishi habari KM alieleza juu ya tukio katika Usomali, ambapo Alkhamisi asubuhi, magari mawili yaliochorwa alama ya UM, yaliripotiwa kutumiwa kwenye shambulio la kujitoa mhanga liliofanyika kwenye kambi ya wanajeshi wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika (AMISOM) katika mji mkuu wa Mogadishu.