Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM anahimiza ushirikiano wa wahusika wengi kusuluhisha matatizo ya kimataifa

KM anahimiza ushirikiano wa wahusika wengi kusuluhisha matatizo ya kimataifa

KM Ban Ki-moon, kwenye mahojiano yake ya kila mwezi katika Makao Makuu, na waandishi habari wa kimataifa, alitilia mkazo haja kuu ya kufufua upya ushirikiano wenye wahusika wengi, ili kukabiliana vyema na matatizo yalioupamba ulimwengu kwa hivi sasa,

ikijumlisha matatizo ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa, mizozo ya kiuchumi pamoja na masuala juu ya upunguzaji wa silaha, kwa ujumla, mada ambazo zitazingatiwa kwenye kikao cha mwaka huu cha Baraza Kuu la UM. KM alisema mwaka huu ni muhimu sana ambapo Mataifa Wanachama yatahitajia "vitendo vya maamuzi hakika juu ya matatizo kadha yalioukabili ulimwengu."