Mashirika ya UM yamuunga mkono KM na rai ya kuanzisha idara maalumu kwa masuala ya kijinsiya

16 Septemba 2009

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu (UNIFEM) pamoja na Jumuiya Mashirika ya UM Kupambana na UKIMWI (UNAIDS) yameripoti kuunga mkono ile rai ya KM ya kufungamanisha vitengo vya UM vinavyohusika na masuala ya wanawake kuwa Idara moja.

Jumuiya ya UNAIDS ilieleza kwamba asilimia kubwa isiowiana ya wanawake ndio yenye kuteseka na maambukizi ya janga la UKIMWI ulimwenguni. UNAIDS imeahidi kuwa itajihusisha kikamilifu na shirika jipya la UM, kuendeleza huduma muhimu za uzazi na afya ya watoto wachanga kwa wanawake na watoto wa kike katika kiwango cha umma.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter