Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya vifo kupanda kwa wahamiaji Waafrika waliojaribu kuvuka Ghuba ya Aden

Idadi ya vifo kupanda kwa wahamiaji Waafrika waliojaribu kuvuka Ghuba ya Aden

Mnamo saa 48 zilizopita imeripotiwa na Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) kwamba watu 16 walifariki na 49 wengine wamepotea, na kudhaniwa ni maututi kwa sababu ya matukio matatu tofauti yanayoambatana na mashua zilizokuwa zikivusha watu kimagendo kwenye Ghuba ya Aden wahamiaji waliojumlisha wale waliotoka Usomali na raia wengine wa kutoka Afrika.

Tukio la kwanza lilisajiliwa kujiri Ijumapili asubuhi nje ya mwambao wa Radfan, kilomita 150 mashariki ya kituo cha kupokea wahamiaji cha Mayfa. Mtu mmoja aliyesalimika kuzama aliwaambia maofisa wa UNHCR Yemen kwamba abiria kadha walipokuwa wanavushwa walipigwa mikwaju mara kwa mara na wafanya magendo na kutishiwa kutupwa baharini.