BK limepitisha azimio juu ya 'haki ya kulinda raia'

15 Septemba 2009

Baraza Kuu la UM limepitisha, kwa pamoja, lile Azimio la \'Wajibu wa Mataifa Kulinda Raia\' wakati wajumbe wa kimataifa walipokaribia kufunga kikao cha 63 katika Ijumatatu alasiri.

KM kwenye taarifa aliotoa, kwa kupitia ofisi ya msemaji wake, alisistiza kwamba hatua iliochukuliwa na Baraza Kuu ilikuwa ni "muhimu sana .. katika kuyaongoza mataifa kwenye utekelezaji wa ahadi ziliofikiwa katika Mkutano Mkuu wa Dunia wa 2005, mkutano ambao ulikusudiwa kuuhifadhi umma wa kimataifa na majanga yanayohusikana na mauaji ya halaiki, makosa ya vita, umezwaji wa kimataifa, na makosa ya jinai dhidi ya utu". Alitumai mafanikio yatapatikna miongoni mwa wajumbe wa kimataifa, kwenye majadiliano yatakayofanyika siku zijazo yenye lengo la kutafuta taratibu za kuridhisha juu ya namna ya kutekeleza mapendekezo ya azimio, kwa kulingana na mapendekezo yaliojadiliwa mwezi Juni kwenye Baraza Kuu la UM.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter