Baraza la Haki za Binadamu laanzisha kikao cha kawaida Geneva

14 Septemba 2009

Baraza la Haki za Binadamu leo limeanza rasmi kikao chake cha kawaida cha kumi na mbili mjini Geneva. Mkutano ulianza kwa majadiliano ya hadhi ya juu ambapo wawakilishi wa Sri Lanka, Marekani na Thailand walihutubia.

Mnamo tarehe 29 Novemba Baraza la Haki za Binadamu litazingatia matokeo ya ujumbe wa kutafuta ukweli juu ya taathira ya mashambulio ya Tarafa ya Ghaza, uliongozwa na Jaji Richar Goldstone wa Afrika Kusini.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter