Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa IAEA apendekeza taasisi yao ipatiwe madaraka zaidi kuendeleza shughuli zake

Mkuu wa IAEA apendekeza taasisi yao ipatiwe madaraka zaidi kuendeleza shughuli zake

Kadhalika, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la IAEA, Mohamed ElBaradei kwenye risala alioitoa mbele ya kikao cha 53 cha Baraza Kuu la IAEA alizisihi nchi wanachama kuipatia taasisi yao "madaraka zaidi ili kuzuia kihakika, na kwa mafanikio, uenezaji wa silaha za kinyuklia katika ulimwengu" hususan kwenye usimamizi wa utekelezaji wa kanuni za Mkataba wa NPT.

Alisema Shirika la IAEA halitofanikiwa kutekeleza shughuli zake kwa upweke, kwa sababu linahitajia mchango unaoaminika na msaada wa kisiasa wa kisiasa kutoka Baraza la Usalama." Hata hivyo, ElBaradei aliliomba Baraza la Usalama kubuni "utaratibu wa jumla wenye makubaliano yasiotegemea vikwazo dhidi ya taifa linalodaiwa kukiuka kanuni za NPT," kwa sababu vikwazo, alitilia mkazo, mara nyingi huwadhuru zaidi watu walio dhaifu na wasio hatia.