UNESCO imemteua Paul Ahyi wa Togo kuwa msanii mpya wa kutetea amani

11 Septemba 2009

Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Alkhamisi limemteua msanii wa kutoka Togo, anayeitwa Paul Ahyi kuwa mwanachama mpya wa orodha ya watu mashuhuri wanaotumia sauti zao, vipaji na hadhi walizonazo kusaidia kutangaza ujumbe wa UNESCO ulimwenguni, na kuendeleza miradi ya taasisi hii ya UM kimataifa.

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Koïchiro Matsuura Alkhamisi, kwenye taadhima maalumu iliofanyika mjini Paris, alimteua Ahyi kuwa Msanii wa Amani kwa lengo la kuendeleza maadili ya UNESCO kwa kutumia ujuzi wake wa kisanii. Ahyi amepata shahada ya usanii kutoka Chuo cha Sanaa cha Taifa cha Paris na anajulikana kimataifa kwenye ustadi wa ufinyanzi, utengenezaji wa vito na upambaji wa ndani ya majumba.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter