Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Usomali azuru Somaliland

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Usomali azuru Somaliland

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah Alkhamisi alizuru Somaliland ambapo alipata fursa ya kukutana na viongozi wa huko kwa majadiliano kuhusu mpango wa amani na mfumo wa uchaguzi kwenye eneo, pamoja na kusailia masuala kadha mengine muhimu.

Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na ofisi ya raisi wa Somaliland Ould-Abdallah alitangaza kwamba "UM utafungua ofisi mpya itakayoshughulikia masuala ya kisiasa katika mji wa Hargeisa ... ofisi ambayo inatarajiwa kuchangisha mchango muhimu wa UM utakaoisaidia Somaliland kudhibiti bora usalama wa maeneo yao ya baharini na kukabiliana na ugaidi."