Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jaji mpya kutoka Urusi kuapishwa na ICTR

Jaji mpya kutoka Urusi kuapishwa na ICTR

Mnamo siku ya leo, kwenye Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) iliopo Arusha, Tanzania aliapishwa Jaji mpya wa kutoka Shirikisho la Urusi, Bakhtiyar Tuzmukhamedov.

Jaji Tuzmukhamedov, mwenye umri wa miaka 54 alikuwa ni Mshauri wa Mahakama ya Katiba ya Urusi kuanzia 1992. Vile vile kuanzia 1984 Jaji Tuzmukhamedov alikuwa Profesa wa Sheria za Kimataifa kwenye Chuo cha Diplomasiya cha Moscow cha Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi. Jaji Tuzmukhamedov pia ameshika nafasi kadha nyenginezo zinazohusu sheria, amechapisha vitabu na makala mbalimbali juu ya sheria za kimataifa. Kuhusu masomo, Jaji Tuzmukhamedov alipata shahada za sheria kutoka Taasisi ya Taifa ya Moscow juu ya Uhusiano wa Kimataifa na katika Chuo Kikuu cha Sheria cha Harvard, Marekani.