Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM anahadharisha juu ya hatari ya ulimwengu uliofurika silaha

KM anahadharisha juu ya hatari ya ulimwengu uliofurika silaha

KM Ban Ki-moon leo amefungua rasmi kikao cha 62 cha Mkutano wa Idara ya Mawasiliano ya Umma (DPI)-na Mashirika Yasio ya Kiserikali (NGOs) katika Mexico City, Mexico.

Kwenye hotuba yake ya ufunguzi alihadharisha kwamba "ulimwengu umejirundika, kwa wingi zaidi, jumla ya silaha zilizokiuka mpaka wakati huduma za amani zinaendelea kufadhiliwa mchango wa fedha haba kabisa." Wakati huo huo matumizi ya kwenye shughuli za kijeshi yanazidi kupanda na kuongezeka na kukiuka jumla ya dola trilioni moja kila mwaka. Lakini KM alisema anashukuru mchango adhimu, wa utetezi, wa mashirika yasio ya kiserikali yaliofanikiwa, hivi sasa, kurudisha tena yale majadiliano ya kupunugza silaha, upya, kwenye ajenda za kimataifa. Alisema mchango wa mashirika haya yasio ya kiserikali utasaidia pakubwa kukomesha utengenezaji wa silaha maututi na haribifu dhidi ya umma wa kimataifa.