UNEP na Kenya waomba msaada wa kufufua misitu ya Mau

9 Septemba 2009

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) limetoa mwito unaopendekeza kuchangishwa msaada wa dharura, wa mamilioni ya dola, utakaotumiwa kufufua na kutengeneza Maeneo ya Misitu ya Mau katika Kenya.

Maeneo ya Misitu ya Mau yanajumlisha hekta 400,000 za funiko la msitu wenye mfumo wa ikolojia uliojifungafunga, ambapo eneo lake linakadiriwa kuwa sawa na eneo la mchanganyiko wa Mlima Kenya na safu ya milima ya Aberdares. Kwa mujibu wa risala ya Mkurugenzi Mkuu wa UNEP, Achim Steiner "Maeneo ya Misitu ya Mau ni muhimu kabisa katika udhibiti wa muda mrefu wa maendeleo ya uchumi, jamii pamoja na ikolojia ya sasa hivi na ya siku zijazo katika Kenya." Alisema UNEP itashirikiana kwa njia zote na Serikali ya Kenya katika utekelezaji wa kadhia hizo muhimu.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter