Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Naibu Katibu Mkuu Asha-Rose Migiro anasailia miaka miwili ya utendaji kazi katika UM

Naibu Katibu Mkuu Asha-Rose Migiro anasailia miaka miwili ya utendaji kazi katika UM

Dktr Asha-Rose Migiro, raia wa Tanzania, alianza kazi rasmi ya NKM wa UM mnamo tarehe mosi Februari 2007. Alikuwa ni NKM wa tatu kuteuliwa kuchukua nafasi hii tangu ilipoanzishwa rasmi katika 1997.

Mtayarishaji vipindi wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM, AZR, alipata fursa ya kufanya mazungumzo kwenye studio za UM na NKM mnamo siku ya Alkhamisi ambapo Bi Migiro alitupatia fafanuzi za jumla kuhusu majukumu anayokabiliwa nayo kwenye utendaji wa kazi hapa Makao Makuu.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.