Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

hapanapale

 Ripoti mpya ya KM, inayotolewa kila miezi mitatu, juu ya shughuli za Ofisi ya UM Inayohusika na Ujenzi wa Huduma za Mchanganyiko za Amani katika Sierra Leone (UNIPSIL) iliowasilishwa Alkhamisi, ilisailia hali nchini katika miezi ya Juni mpaka Septemba 2009. Ripoti ilieleza mazingira ya kisiasa, kwa ujumla, yamesalia kuwa shwari katika taifa na hakujatukia fujo za kisiasa katika kipindi hicho. Lakini ripoti ilisisitiza juu ya umuhimu wa kukabili mapema hali ya kutovumiliana kisiasa iliojiri ndani ya nchi, kwa sababu ya uwezekano wa fujo kufufuka tena kieneo, hususan kwenye kile kipindi ambapo vyama vya kisiasa vitakapokuwa vinajiandaa kugombania uchaguzi wa 2012. Ripoti ilihadharisha pia maamirisho ya hali ya usalama ndani ya nchi ni kadhia inayohatarishwa kuzorotishwa, kwa sababu ya ukosefu mkubwa wa ajira kwa vijana na shughuli haramu za biashara ya madawa ya kulevya. Vile vile KM aliihimiza jumuiya ya kimataifa kuusaidia umma wa Sierra Leone kukabiliana kidharura na masuala muhimu ya kukomesha viwango vikubwa vya vifo vya watoto wachanga na vifo vya uzazi ambayo huathiri maendeleo yao.