Mahakama ya Rufaa ya ICC imeamua aliyekuwa kiongozi wa JKK asalie kizuizini wakati akisubiri kesi

3 Septemba 2009

Mahakama Ndogo ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa Juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) imeamua Jean-Pierre Bemba Gombo, aliyekuwa Naibu Raisi wa JKK, aendelee kuwekwa kifungoni kabla ya kesi yake kusikilizwa na Mahakama Kuu.

 Bemba alituhumiwa kufanya makosa ya vita na jinai dhidi ya utu - ikijumlisha vitendo haramu vya kunajisi watu kimabavu, mauaji ya kihorera na pia uchukuwaji wa ngawira - vitendo vilivyofanyika katika taifa jirani la Jamhuri ya Afrika ya Kati mnamo miaka ya 2002 na 2003. Mahakama Ndogo ya Kusikiliza Mashtaka kabla ya kesi mwezi uliopita ilipendekeza Bemba aachiwe kwa muda na kwa masharti, mpaka pale kesi yake itakaposikilizwa. Lakini Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama ya ICC, Luis Oreno Ocampo aliomba uamuzi huo usitekelezwe kwa kukhofia mtuhumiwa huenda akakimbia na kuwadhuru raia waliotayarishwa kutoa ushahidi dhidi yake.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter