Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa WCC3 waafikiana kuanzisha mfumo mpya wa kuhudumia utabiri wa hali ya hewa

Mkutano wa WCC3 waafikiana kuanzisha mfumo mpya wa kuhudumia utabiri wa hali ya hewa

Mkutano Mkuu wa Tatu juu ya Hali ya Hewa (WCC3) unaokutana hivi sasa Geneva, Alkhamisi ulipitisha Mwito wa Azimio la kuanzisha Mfumo Mpya wa Dunia Kuhudumia Utabiri wa Hali ya Hewa, utaratibu ambao utayawezesha Mataifa Wanachama kupata taarifa, kwa wakati, kuhusu mageuzi katika hali ya hewa.

Michel Jarraud, Mkuu wa Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) alisema Mkutano wa WCC3 ulikuwa wa mafanikio baada ya wabuni-sera wa viwango vya juu vya madaraka, kutoka nchi 150, kupitisha azimio la Mfumo Mpya wa Kuhudumia Hali ya Hewa, wakiwemo viongozi wa Afrika Wakuu wa Taifa/Serikali kutoka Ethiopia na Msumbiji pamoja na ManaibuRaisi wa Visiwa vya Comoro na Tanzania, na kujumlisha pia Mawaziri na Maofisa Wakuu wengine wa Serikali zaidi ya 80. Mfumo wa Kutabiri Hali ya Hewa unatarajiwa kutekelezwa kwa kiawamu, na utaanza kutumika katika 2011. Lengo la utaratibu huu ni kuyasaidia Matifa Wanachama, hususan zile nchi maskini, kumudu, kudhibiti bora pamoja na kujirekibisha na mazingira mapya yanayoletwa na taathira za mabadiliko ya hali ya hewa katika ulimwengu. Mkutano wa WCC3 ulianza majadiliano yake tarehe 31 Agosti na unatazamiwa kuhitimishwa Ijumaa Septemba 04 (2009).