Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji wa katika mifumo ya ikolojia una matumaini ya kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa, inasema TEEB

Uwekezaji wa katika mifumo ya ikolojia una matumaini ya kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa, inasema TEEB

Matokeo ya mradi ulioanzishwa na Ujerumani pamoja na Kamisheni ya Mataifa ya Ulaya kuhusu masuala ya hali ya hewa, unaosimamiwa na Taasisi juu ya Uchumi wa Mfumo wa Ikolojia na Viumbe Hai Anuwai (TEEB), yamethibitisha dhahiri kwamba uwekezaji kwenye huduma za kufufua mifumo ya ikolojia ni hatua yenye uwezo mkubwa wa kudhibiti bora taathira za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni, na ni hatua itakayoimarisha uchumi wa kimataifa, halkadhalika, pindi itatekelezwa kama inavyostahiki.

Mifumo ya ikolojia ya Dunia ikipatiwa mitaji ya kuridhisha, ilisema taarifa ya Tassisi ya TEEB, ina uwezo wa kuzalisha mapato ya trilioni ya madola, kutokana na udhibiti bora wa shughuli za misitu, harakati za maeneo chepechepe ya matopetope na kwenye mabonde ya mito. Uchunguzi wa Taasisi ya TEEB ulifanyika baada ya kugunduliwa kwamba mfumo wa viumbe hai anuwai na "mioundumbinu ya ikolojia" huwa inahatarishwa kupotea, kwa sababu ya kuongezeka kwa hewa chafu kwenye anga. Utafiti uliidhinishwa na Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP).