Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM ahimiza mataifa kukamilisha maafikiano ya Mkutano Mkuu juu ya taathira za hali ya hewa

KM ahimiza mataifa kukamilisha maafikiano ya Mkutano Mkuu juu ya taathira za hali ya hewa

KM Ban Ki-moon amewasihi walimwengu kuchukua hatua za dharura ili kukabiliana haraka na athari chafuzi za mabadiliko ya hali ya hewa, na kuyahifadhi maisha ya vizazi vijavyo.

 Ombi hili lilitolewa Ijumanne wakati KM alipokuwa anazuru ukingo wa ncha ya Kaskazini ya dunia, kwenye eneo la Akitiki, ambapo alishuhudia binafsi kuyayuka kwa kasi, kwa miamba ya barafu na michirizi ya mabarafu kutokana na athari za mabadiliko katika hali ya hewa duniani. Alitahadharisha KM ya kwamba wakati hatunao tena, na ni wajibu kwa Mataifa Wanachama yote kufanya kila wanavyoweza "kukamilisha makubaliano ya Mkutano Mkuu wa Copenhagen, Denmark kuhusu udhibiti wa mabadiliko ya hali ya hewa," maafikiano ambayo alitilia mkazo yawe ya jumla, ya haki na yalio sawia, ili kuhakikisha nchi zenye maendeleo ya viwandani pamoja na nchi zinazoendelea, na vile vile umma wote wa kimataifa, kwa pamoja watapatiwa fursa ya kuishi kwenye mazingira salama