Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanajeshi wa Rwanda akabidhiwa madaraka ya Kamanda Mkuu mpya kwa Darfur

Mwanajeshi wa Rwanda akabidhiwa madaraka ya Kamanda Mkuu mpya kwa Darfur

Kamanda Mkuu mpya wa Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) kutoka Rwanda, Liuteni-Jenerali Patrick Nyamvumba ameripotiwa kuanza kazi rasmi hii leo.

Aliwasili Darfur tarehe 24 Agosti na alichukua fursa hiyo ya kuzuru, kwa kujijulisha, watumishi raia na wanajeshi wa UNAMID. Jenerali Nyamvumba alichaguliwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) na KM wa UM kumrithi Jenerali Martin Luther Agwai, aliyekuwa Kamanda Mkuu wa kwanza wa UNAMID tangu taasisi hii ilipoanzishwa miaka ya nyuma.