Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano makali Mogadishu yanaathiri zaidi raia, inasema OCHA

Mapigano makali Mogadishu yanaathiri zaidi raia, inasema OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kutoka Geneva kwamba mapigano makali yaliopamba kwenye mji wa Mogadishu, Usomali yanaendelea kuathiri kwa wingi raia.

Taarifa za OCHA zinaeleza kwamba wiki hii pekee raia 50 waliuawa kwa sababu ya mapigano, na wakati huo huo darzeni kadha za watu walijeruhiwa kutokana na mapambano baina ya vikosi vya serikali na makundi ya wapinzani. Watu milioni 3.8 - sawa na nusu ya idadi ya watu nchini Usomali - wanahitajia kufadhiliwa misaada ya kiutu pamoja na utaratibu wa kupata kazi halali ili kuweza kumudu maisha ya kawaida. Kwa mujibu wa makadirio ya OCHA, asilimia 75 ya umma muhitaji umekusanyika, na hukutikana hasa kwenye zile sehemu za Usomali za kati na kusini, maeneo ambayo ndipo mapigano yaliposhtadi kwa nguvu zaidi, na kusababisha watu kupoteza maisha, ajira kutoweka na kuzorotisha juhudi za mashirika ya kimataifa yanayogawa misaada ya kiutu kwa raia muhitaji.