Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisa wa UNHCR anasailia mzozo wa makazi kwenye kambi za wahamiaji za Dadaab, Kenya

Ofisa wa UNHCR anasailia mzozo wa makazi kwenye kambi za wahamiaji za Dadaab, Kenya

Katika miezi ya karibuni, vurugu na mizozo ya kihali ilikithiri kwa wingi katika Usomali, hali iliosababaisha maelfu ya raia kuamua kuhama makwao na kuelekea mataifa jirani kutafuta hifadhi na usalama.

Mathalan, tangu mwezi Januari mwaka huu, wahamiaji 43,000 wa Usomali walisajiliwa na mashirika ya kimataifa kuomba hifadhi kwenye kambi za wahamaiji za Dadaab, katika Kenya. Mtiririko huu wa watu ulisababisha matatizo makubwa katika operesheni za UM za kuwahudumia wahajirina hawa mahitaji yao ya kimsingi. Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) ambalo hushughulikia kadhiahizo, limeamua kuwahamisha baadhi ya wahamiaji kutoka kambi zilizofurika za Dadaaba na kuwapeleka kwenye sehemu nyengine za Kenya ambapo mahitaji yao yataweza kuhudumiwa vyema.

Karibuni mtayarishaji vipindi vya Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM, AZR, alipata fursa ya kuzungumza na ofisa mkazi wa UNHCR katika Kenya, anayeitwa Yussuf Hassan. Kwenye mahojiano yao, Ofisa huyu alitupatia fafanuzi halisi kuhusu tatizo la wahamiaji waliopo Dadaab, na kuelezea namna UM unavyojitahidi kulitatua suala hili kwa suluhu ya kuridhisha.

Sikiliza taarifa kamili kwenye idhaa ya mtandao.