Marehemu Seneta E. Kennedy wa Marekani aombolezwa na KM na UNHCR

Marehemu Seneta E. Kennedy wa Marekani aombolezwa na KM na UNHCR

Viongozi wa UM leo walitoa shukrani kadha na kumkumbuka kidhati seneta wa Marekani, Edward Kennedy ambaye alifariki Ijumanne usiku akiwa na umri wa miaka 77 baada ya kuugua saratani ya ubongo kwa muda mrefu.

Walimsifu kwa mchango wake katika kuhami haki za umma dhaifu wa kimataifa. KM Ban Ki-moon kwenye taarifa yake alisema Seneta Kennedy alikuwa miongoni mwa watetezi wa nguvu wa UM, na alimpatia KM ushauri uliojaa busara katika kuongoza kazi zake. Alisema Seneta Kennedy alitetea zaidi haki na masilahi ya umma uliokosa kinga na ulinzi. Kamishna Mkuu wa UM juu ya Huduma za Wahamiaji, António Guterres, yeye kwa upande wake alisema maisha ya Seneta Kennedy ni ushahidi wenye kuthibitisha dhahiri tofauti ya kimaisha kwa umma, inayoweza kutekelezwa na mtungasera mmoja pekee. Alisema Seneta Kennedy alikuwa ni mtetezi asiyechoka ambaye kwa karibu miaka khamsini alipigania sheria kadha zilizotungwa kutekeleza haki za wahamiaji na wale wenye kuomba hifadhi za kisiasa, kwa kukomesha ubaguzi dhdi yao.