Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia wanaohitajia lishe na misaada ya kiutu imekithiri Usomali: FSNAU

Raia wanaohitajia lishe na misaada ya kiutu imekithiri Usomali: FSNAU

Kitengo cha UM Kinachotathminia Lishe na Akiba ya Chakula katika Usomali (FSNAU) kimeripoti kwamba tangu mwezi Januari 2009, idadi ya watu wenye kuhitajia misaada ya kihali na fursa ya kupata ajira nchini Usomali imeongezeka kwa asilimia 18, kutoka watu muhitaji milioni 3.7 na kufikia watu milioni 3.57, sawa na nusu ya idadi ya watu wa katika taifa hilo la Pembe ya Afrika.

Takwimu zimeonyesha mizozo ya kiutu iliofumka Usomali imeathiri watu wa vijijini milioni 1.4 ambao wamebanwa na janga la ukame, wakijumuika na wakazi wa miji 650,000, na wahamiaji wa ndani ya nchi milioni 1.4 waliohajiri makazi yao kunusuru maisha. Kitengo cha FSNAU, kinasimamiwa na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO). Ripoti ilionyesha asilimia 75 ya watu milioni 3.76 waliokabiliwa na mizozo hii ya kihali wanakutikana katika maeneo ya kusini na ya kati nchini Usomali - sehemu ambazo katika siku za karibuni mapigano makali yalishtadi, na kuwazuia wahudumia misaada ya kiutu kuendeleza operesheni za kugawa misaada ya chakula na mahitaji mengine ya kiutu kwa umma husika.