Siku ya Kumbukumbu ya Kimataifa juu ya Taathira za Utumwa

24 Agosti 2009

Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya Ukomeshaji wa Biashara ya Utumwa huadhimishwa na UM kila mwaka mnamo tarehe 23 Agosti.

Kwenye risala iliotolewa na Koïchiro Matsuura, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwenye taadhima za mwaka huu za Siku hiyo, aliangaza juuya ile raia inayotilia mkazo umuhimu wa walimwengu kuungana "kimawazo, kwa uwiano wa kihistoria kuhusu biashara ya utumwa na utumwa, wenyewe na kukumbushana tena, kwa busara inayoona mbali, ya kwamba kama wanadamu tunawajibika kuweka misingi ya majadiliano yenye natija kwa umma wote wa kimataifa, ili tuimarishe maarifa kuhusu jadi yetu moja ya ubinadamu na kukuza taaluma za kuvumiliana kitamaduni."

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter