Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa mkataba wa kudhibiti silaha za kibayolojia wanakutana Geneva

Wataalamu wa mkataba wa kudhibiti silaha za kibayolojia wanakutana Geneva

Wataalamu magwiji wa fani ya silaha zinazotumia vijidudu vya viumbehai wanakutana hivi sasa mjini Geneva kusaillia maendeleo katika ujenzi wa fani ya uchunguzi wa maradhi ya vijidudu hivyo, ugunduzi wake, utambuzi wa ugonjwa na udhibiti wake.

Mkutano umekusudiwa hasa kuimarisha Mkataba wa kudhibiti bora silaha za vijidudu vinavyotengenezwa viumbe hai na kuendeleza, kwa ufanisi, jitihadi za kukomesha kikamilifu silaha hizo. Mkataba huo, unaojulikana kwa umaarufu kama Mkataba wa BWC, umepiga marufuku kwa taifa kuendeleza huduma za kuzalisha silaha za viumbe hai, au kurimbikiza silaha za sumu za vijidudu hivyo kwenye maghala yao ya silaha.