Skip to main content

Mkutano wa Stockholm wasisitiza ulazima wa kujumuisha suala la maji kwenye kikao cha COP-15

Mkutano wa Stockholm wasisitiza ulazima wa kujumuisha suala la maji kwenye kikao cha COP-15

Wajumbe walioshiriki kwenye mkutato unaoadhimisha Wiki ya Maji Duniani kwa 2009, unaofanyika kwenye mji wa Stockholm, Sweden wamepitisha hii leo kwa kauli moja azimio linalosema suala la maji ni laizma kujumlishwa kwenye kikao cha COP-15,

 yaani ule mkutano mkuu wa kujadilia mabadiliko ya hali ya hewa duniani utakaofanyika kwenye mji wa Copenhagen mnamo mwisho wa mwaka. Wawakilishi wa jumuiya kadha na maofisa wa mashirika yanayohusika na hifadhi kinga za mazingira wamesisitiza kwenye risala zao juu ya umuhimu wa kujumlisha suala la maji kwenye mahojiano yanayohusu udhibiti wa mabadiliko ya hali ya hewa.