Skip to main content

Maofisi wa polisi wa Jordan, Namibia na Philippines wawasili Darfur kujiunga na UNAMID

Maofisi wa polisi wa Jordan, Namibia na Philippines wawasili Darfur kujiunga na UNAMID

Shirika la Ulinzi Amani la Vikosi vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) wiki hii limepokea kundi la awali la maofisa wa polisi kutoka Jordan, waliowasili Ijumanne kwenye jimbo hilo la Sudan magharibi. Maofisa wa polisi 280 waliosalia kutoka Jordan wanatarajiwa kuwasili Darfur mwisho wa Agosti, na wataenezwa kwenye sehemu za El Fasher na Kabkabiya, Darfur Kaskazini.

Kadhalika Ijumanne waliwasili Darfur maofisa ziada wa polisi 9 kutokea Philippines, pamoja na maofisa wengine 8 raia wa Namibia. Majukumu ya polisi hawa yatakuwa ni kuwahifadhi raia waliopo Darfur, na kuyasaidia mashirika ya kimataifa yanayoshughulikia misaada ya kiutu kuendeleza shughuli zao kwa usalama, na vile vile kuhakikisha sheria za nchi huwa zinafuatwa na kuhishimiwa na makundi husika yote yaliopo kwenye jimbo la mtafaruku la Sudan magharibi.