Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yahadharisha, Sudan Kusini inakabiliwa na upungufu mkubwa wa huduma za kimsingi

UM yahadharisha, Sudan Kusini inakabiliwa na upungufu mkubwa wa huduma za kimsingi

Kuhusu operesheni nyengine za ugawaji chakula katika Sudan, Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kwamba tangu Maafikiano ya Jumla ya Amani yalipotiwa sahihi 2003 na makundi husika na mapigano Sudan Kusini, watu milioni 2.4 waliweza kurejea makwao. Lakini eneo hili, kwa kulingana na taarifa za WFP, ni moja ya sehemu masikini sana katika Afrika, na kuna ukosefu mkubwa wa huduma za kimsingi, kwa ujumla, kwa wakazi wake bado wanasubiri kushuhudia kile kinachotambuliwa kama "mgawo wa natija za amani".