UM umepokea chini ya nusu ya maombi ya msaada unaohitajika Zimbabwe

19 Agosti 2009

Mratibu wa misaada ya kiutu ya UM katika Zimbabwe, Augustino Zacarias ametoa taarifa iliotahadharisha kwamba "ijapokuwa Zimbabwe haikabiliwi na mapigano au vurugu, hata hivyo matishio ya kihali, mathalan, upungufu wa chakula, miripuko ya maradhi ya kuambukiza kama kipindupindu, ni matatizo ambayo bado yanaendelea kusumbua taifa."

  Alisema ombi la UM kwa wahisani wa kimataifa kuisaidia Zimbabwe kifedha, ili iweze kukidhi mahitaji ya umma, kadhia hiyo ilifanikiwa kuchangisha asilimia 44 tu ya dola milioni 718 katika mwisho wa mwezi Julai, fedha ambazo zinazohitajia kutekeleza miradi hiyo ya kiutu kidharura nchini. Kwa kuambatana na takwimu za UM, watu milioni sita katika Zimbabqwe hawana uwezo wa kuwa na nadhafa ya kutunza afya na vile vile wamenyimwa uwezo wa kupata maji safi na salama, matatizo ambayo ndio yaliochochea miripuko ya maambukizi ya maradhi ya kipindupindu mwaka jana, ambapo watu 99,000 walipatwa nayo na kuua wagonjwa 4,000.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter