Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watumishi wawili wa UM, miongoni mwa waliouawa na shambulio la kujiangamiza Afghanistan

Watumishi wawili wa UM, miongoni mwa waliouawa na shambulio la kujiangamiza Afghanistan

Watumishi wawili wa UM katika Afghanistan walikuwa miongoni mwa watu saba waliouawa, Ijumanne ya leo, shambulio la bomu la kujitolea mhanga liliotukia katika sehemuya kati ya mji wa Kabul, siku mbili kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa taifa kuteua wawakilishi wa baraza la majimbo na raisi.

Kai Eide, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Afghanistan na Mkuu wa Shirika la Usaidizi Amani la UM katika Afghanistan (UNAMA) amenakiliwa akisema kwenye taarifa alioitoa baada ya tukio hili kwamba "ameshtushwa na kuhuzunishwa sana kujua wafanyakazi wake wawili walikuwa miongoni mwa wale waliouawa na shambulio la kujitolea". Eide aliwalaani "kikamilifu wale waliohusika na kitendo hiki cha jinai." Mfanyakazi wa tatu wa UM naye pia alijeruhiwa kwenye shambulio hilo, na sasa hivi anapata matibabu ya majeraha yake Kabul.