Skip to main content

Waathirika wa chuki za wageni Afrika Kusini wanasema 'bora usalama badala ya anasa za maisha'

Waathirika wa chuki za wageni Afrika Kusini wanasema 'bora usalama badala ya anasa za maisha'

Taarifa ya Ofisi ya UM juu ya Huduma za Dharura (OCHA) iliotolewa wiki hii ilielezea mvutano uliozuka kwenye kambi ya makazi ya muda ya Bluewater, katika mji wa Cape Town ambapo wanaishi wahamiaji 396 ambao mnamo mwezi Mei 2008 walifukuzwa kwenye mastakimu ya muda kwa sababu ya tukio liliodaiwa kuwakilisha chuki za wazalendo dhidi ya wageni.

Ripoti zilizopokewa na Ofisi ya OCHA zinasema mnamo tarehe 11 Agosti 2009, Arnoldus Smit, kaimu jaji wa Mahakama Kuu Afrika Kusini aliamuru kusitishwa, kwa muda, ile hukumu ya kuwafukuza wahamiaji hawo kutoka makazi yao ya muda ya Bluewater, hukumu ambayo inaambatana na ombi la serikali ya Jiji la Cape Town.  Jaji Smit alichukua uamuzi huu baada ya kuarifiwa makundi mawili husika na mvutano wa kambi ya Bluewater, yalikaribia kufikia mapatano ya kuridhisha. Kwa mujibu wa taarifa za OCHA, Jiji la Cape Town linataka wahamiaji wageni wasitengwe kwenye maskani mbali na jamii za Afrika Kusini, na ilipendekeza wageni hawa wachanganyishwe na jamii za kawaida za yale maeneo waliyoyakimbia, baada ya kuzuka fujo dhidi ya wageni mwaka jana.

Sikiliza taarifa kamili kutoka idhaa ya mtandao.