Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhamisho wa mabavu wa raia katika Port Harcourt, Nigeria waitia wasiwasi UM

Uhamisho wa mabavu wa raia katika Port Harcourt, Nigeria waitia wasiwasi UM

Raquel Rolnik, mtaalamu huru wa UM anayetetea haki za umma kupata makazi, ameripoti kutoka Geneva kuingiwa wasiwasi juu ya taarifa alizopokea za kuhamishwa kwa nguvu mamia elfu ya raia waliopo katika Bandari ya Harcourt (Port Harcourt), Nigeria ikiwa miongoni mwa vitendo vya utekelezaji wa sera za serikali za kufufua upya miji.

Kwa mujibu wa Rolnik "matumizi ya nguvu ya kufukuza raia makazi, huruhusika kwenye hali ya aina ya pekee, na isio ya kawaida" pindi wenye madaraka watazingatia kikamilifu, sheria ya kimataifa ambapo watu wanaovunjiwa makazi huwa na haki ya kulipwa fidia. Kadhalika, waathirika hawa wana haki ya kupata hifadhi ya kisheria, ikijumlisha haki ya kupewa ushauri unaoaminika na wenye madaraka, pamoja na kupewa taarifa ya mapema juu ya kubomolewa kwa makazi yao, na baadaye kufadhiliwa vile vile hukumu inayoridhisha pamoja na misaada ya kisheria inayoambatana na kanuni za haki za binadamu, kwa kuhakakisha watu wanaohusika na ubomoaji wa nyumba za raia huwa wanajulikana na kutambilika kisheria. Mtetezi wa UM juu ya Haki za Makazi Bora Rolnik, alisema itakuwa ni kinyume na sheria pindi mtu anayebomolewa rasmi makazi, na serikali, hunyimwa makazi mbadala, kitendo ambacho kinatafsiriwa kuharamisha haki za kiutu za kimataifa. Mnamo mwezi Februari 2009, Serikali ya Jimbo la Mtoni katika Nigeria lilitangaza rasmi kuwa litabomoa nyumba zote zilizokabili pwani katika Bandari ya Harcourt, ikiwa miongoni mwa hekaheka ya utekelezaji wa sera ya kufufua upya miji. Tangu wakati huo wenye madaraka wameripotiwa kuvunja kihorera nyumba za raia wa maeneo kadha wa kadha ya Bandari ya Harcourt, na ilhali Mahakama Kuu ya Shirikisho la Nigeria imetoa amri maalumu ya kusimamisha vitendo vya kuwang'oa raia kimabavu kutoka makazi yao halali mpaka wakati suala hili litakaposuluhishwa kisheria na kwa ridhaa ya wote husika.