Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walinzi amani wa Tanzania wawasili Darfur: UNAMID

Walinzi amani wa Tanzania wawasili Darfur: UNAMID

Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) limetangaza kwamba wanajeshi walinzi amani 200 kutoka Tanzania leo wamewasili kujiunga na operesheni zake kwenye jimbo la magharibi la Sudan.

Vikosi hivi vinajumlisha kundi la mwanzo la asari wa Tanzania kuwasili Darfur. Vikosi ziada vinatarajiwa kujiunga na UNAMID mwezi Septemba. UNAMID imetangaza kwamba imefanikiwa hivi sasa kukamilisha asilimia 70 ya wanajeshi na polisi waliodhaminiwa na Baraza la Usalama - sawa na askari 14,180.