Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku Kuu ya Kimataifa kwa Vijana

Siku Kuu ya Kimataifa kwa Vijana

Tarehe ya leo, Agosti 12, inahishimiwa na UM kuwa ni Siku Kuu ya Kimataifa kwa Vijana. Kwenye risala aliotoa kuadhimisha siku hii, KM Ban Ki-moon alikumbusha matatizo yaliowakabili vijana kwa hivi sasa, vijana wa kiume na wa kike duniani, huathiri bila kiasi fungu hili la umma wa kimataifa, kwa sababu ya kuanguka kwa shughuli za uchumi kwenye soko la kimataifa na kutokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Alitoa mfano wa 2007, ambapo takwimu za kimataifa zilithibitisha licha ya kuwa vijana huwa inajumlisha asilimia 25 ya umma wa kimataifa, asilimia 40 ya vijana waliotimia umri wa kufanya kazi huwa hawana kazi, idadi ambayo inaendelea kupanda, hasa katika nchi zinazoendelea. Kadhalika, Thoraya Ahmed Obaid, Mkurugenzi Mkuu wa UM juu ya Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu (UNFPA) kwenye risala aliotoa kuadhimisha Siku Kuu ya Kimataifa kwa Vijana alikumbusha idadi ya vijana hivi sasa ulimwenguni, kati ya umri wa miaka 10 mpaka 25, inajumlisha watu bilioni 1.5, ikiwakilisha idadi kubwa kabisa ya vizazi kihistoria. Alisema kwa ulimwengu kuweza kuwasilisha wizani unaofaa kukabiliana bora na matatizo ya chakula, migogoro ya fedha na athari za mabadiliko ya hali ya hewa duniani, jumuiya ya kimataifa itawajibika kuwekeza zaidi kwenye huduma za kuimarisha afya ya vijana, ilimu bora na uongozi unaoridhisha, na kuhakikisha vijana wanashirikishwa kikamilifu kwenye kadhia hizi.