Skip to main content

Watathminia madawa wanabashiriwa Septemba kuidhinisha chanjo kinga mpya dhidi ya homa ya A/H1N1

Watathminia madawa wanabashiriwa Septemba kuidhinisha chanjo kinga mpya dhidi ya homa ya A/H1N1

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti leo kwamba linatarajia kupata idhini ya taasisi za serikali zinazosimamia utumiaji madawa, kutengeneza kwa wingi mnamo mwezi Septemba dawa ya chanjo kinga dhidi ya homa ya mafua ya A/H1N1.

WHO imesema itaandaa orodha ya namna chanjo hiyo itakavyogawanywa miongoni mwa wahudumia afya wa kimataifa. Huduma za kuchanja watu ni shughuli zinazosimamiwa na serikali, na inatarajiwa taasisi za serikali ndizo zitakazoamua ugawaji wa dawa hizo kwa raia baada ya kuzipokea kutoka UM.