Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres anasema mzozo wa wahamiaji wa Usomali nchini Kenya ni wa "tamthilia"

Guterres anasema mzozo wa wahamiaji wa Usomali nchini Kenya ni wa "tamthilia"

António Guterres, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Huduma za Wahamiaji, wakati alipozuru kambi ya Dadaab wanapoishi wahamiaji wanaobanana wa Usomali robo milioni, kwenye eneo liliotandawaa Kenya ya kaskazini-mashariki, alitoa mwito maalumu kwa jamii ya kimataifa kukithirisha mchango wao wa fedha zinazohitajika kuuhudumia umma huu kihali.

Alikumbusha kwamba mazingira ya kambi ya Dadaab ni "magumu kabisa ulimwenguni kwa wahamiaji wanaotafuta hifadhi". Kambi ya Dadaab ipo kilomita 90 kutoka mpaka na Usomali, na inajumusiha maeneo matatu ambayo yalipojengwa kuwapatia wahamiaji makazi ya muda, yalikusudiwa kupokea watu 90,000 na hivi sasa wahamiaji zaidi ya 250,000 huishi hapo, wingi wao kutokea Usomali. UNHCR imeripoti miondombinu ya makazi ya Dadaab vile vile inahitajia marekibisho ya haraka, hususan kwenye ile mitandao inayohusika na ugawaji wa maji safi pamoja na kwenye zile huduma za kimsingi, zinazohusu ilimu na afya, huduma zote ambazo zinatakiwa kupanuliwa, kukidhi bora mahitaji ya wahamiaji.