Skip to main content

UNHCR inaomba maskani ziada kutoka Kenya kwa wahamiaji wa Usomali

UNHCR inaomba maskani ziada kutoka Kenya kwa wahamiaji wa Usomali

Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) leo alizuru kambi ya wahamiaji ya Dadaab, iliopo katika eneo la Kenya mashariki ambapo wanaishi, kwa kubanana, wahamiaji 250,000 wa Usomali waliohajiri makwao, kufuatia mapigano yaliozuka nchini mwao mnamo miezi ya karibuni.

Guterres yupo Kenya sasa hivi, kwa madhumuni ya kuzungumza na Serikali juu ya uwezekano wa kuipatia UM ardhi ziada, itakayotumiwa kuhamishia wale wahamiaji wa Usomali ambao wanasongomana kwenye kambi ya Dadaab. Kwa mujibu wa taarifa za UNHCR wahamiaji wa Usomali 6,000 huhajiri makwao kila mwezi na kumiminikia Kenya, na wahudumia misaada ya kiutu hawatoweza kuwashughulikia kihali wahamiaji waliopo kwenye kambi ya Dadaab bila ya kuwahamisha kwenye maeneo mengineyo yenye nafasi ya kuridhisha