Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto waliopo vizuizini Rwanda kusaidiwa mawakili na mradi wa UM

Watoto waliopo vizuizini Rwanda kusaidiwa mawakili na mradi wa UM

Kadhalika Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kwamba linaunga mkono, na kuahidi pia kuusaidia ule mradi ulioanzishwa na Wizara ya Utawala wa Sheria ya Rwanda, wa kuwapatia watoto 600 ziada waliomo vizuizini, mawakili wa kuwatetea kesi zao.

Ahadi hii ilitangazwa kwenye taadhima za ‘Wiki ya Msaada wa Kisheria'. Mnamo wiki hii watumishi wa mahakama, polisi wa taifa na mawakili pamoja na maofis wa magereza hukusanyika kukamilisha kiporo cha kesi za watoto wadogo, na vile vile kutathminia hali halisi za watoto wa umri mdogo waliopo vizuizini. Dktr. Joseph Foumbi, Mwakilishi wa UNICEF katika Rwanda amenakiliwa akisema ‘Wiki ya Msaada wa Kisheria' ni "hatua muhimu inayowapatia watoto wanaokwaruzana na sheria za kitaifa haki kutoka mahakama." Dktr Foumbi aliipongeza Serikali ya Rwanda kwa kuchukua hatua hii ya kujaribu kumaliza kesi za watoto wanaotota kwenye majela ya nchi, na vile vile kupongeza maendeleo ya kisheria kitaif baada ya Bunge la kutunga sheria kupitisha Kanuni ya Kusaidia Kisheria, uamuzi utakaoanzisha mfuko maalumu wa kutumiwa kugharamia kesi za umma ulio dhaifu kihali na mali, ikijumlisha watoto wenye umri mdogo.