Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM ameteua Kamanda Mkuu mpya wa UNAMID kutoka Rwanda

KM ameteua Kamanda Mkuu mpya wa UNAMID kutoka Rwanda

KM amewaariifu wajumbe wa Baraza la Usalama kwamba kutokana na maafikiano na Mwenyekiti wa Kamisheni ya UA, wamemteua Liuteni Jenerali Patrick Nyamvumba wa Rwanda kuwa Kamanda Mkuu mpya wa Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID), kuanzia tarehe mosi Septemba, mwaka huu.

Jenerali Nyamvumba atachukua nafasi ya Jenerali Martin Luther Agwai wa Nigeria, ambaye alishika wadhifa wa Kamanda Mkuu wa UNAMID tangu vikosi hivi vya mchanganyiko kuanzisha operesheni zake kwenye Jimbo la Sudan Magharibi la Darfur.