Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suluhu ya kikanda Afrika ndio yenye uwezo wa kukomesha mizozo, inasema BK

Suluhu ya kikanda Afrika ndio yenye uwezo wa kukomesha mizozo, inasema BK

Baraza Kuu (BK) Alkhamisi limepitisha, bila kupingwa, azimio liliobainisha umuhimu wa kutumia utaratibu wa kikanda kuzuia na kusuluhisha mizozo katika bara la Afrika.

Azimio lilisitiza juu ya haja ya kuimarisha fungamano ziliopo kati ya miradi ya maendeleo ya kiuchumi na jamii katika Afrika, kwa upande mmoja, na ile ajenda ya kusawazisha usalama na amani ya bara zima, kwa upande mwengine. Azimio pia lilikumbusha jukumu muhimu la Umoja wa Afrika (UA) na mashirika madogo ya kizalendo katika kukabiliana na masuala yanayohusu usalama na amani katika Afrika. Azimio lilipitishwa kwa kulingana na mapendekezo ya ripoti ya KM juu ya vyanzo vya mizozo katika Afrika, na juhudi za kudumisha amani na maendeleo yanayosarifika, halkadhalika, barani humo.