Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya KM juu ya hali Usomali

Ripoti ya KM juu ya hali Usomali

Ripoti ya KM juu ya Usomali leo imewakilishwa rasmi hapa Makao Makuu. Ndani ya ripoti, KM alibainisha wasiwasi mkubwa alionao kuhusu majaribio ya karibuni ya makundi ya upinzani ya kutaka kupindua, kwa kutumia nguvu, serikali halali ya Usomali.

Ripoti iliisihi jamii ya kimataifa kutopwelewa katika kuisaidia Serikali ya Usomali kuendesha shughuli zake. Ripoti ya KM ilibainisha kwamba licha ya kuwa hali ya usalama nchini Usomali bado ni ya kigeugeu, hata hivyo Serikali ya Mpito bado inajitahidi kuyajumuisha makundi yote ya kiraia, kwenye mazungumzo yao ya kusuluhisha mifarakano ya kisiasa kwa taratibu za amani, taratibu ambazo zimejumuishwa kwenye Maafikiano ya Amani ya Djibouti. KM alishtumu vikali vitendo vya kundi la upinzani la Al-Shabaab vyenye lengo la kuchochea fujo dhidi ya Serikali.