Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwajibikaji wa taifa kulinda raia ni wazo linaloungwa mkono na Pillay

Uwajibikaji wa taifa kulinda raia ni wazo linaloungwa mkono na Pillay

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay ametoa taarifa maalumu iliochangisha maoni ziada kuhusu mjadala unaofanyika wiki hii, hapa Makao Makuu, kuzingatia suala la "Wajibu wa Jumuiya ya Kimataifa Kulinda Raia".

Alisema majadiliano haya ni muhimu na yataisaidia UM kujiandaa vizuri zaidi kukabiliana na yale matatizo yaliowalazimisha walimwengu, mnamo miaka ya nyuma, kubuni chombo cha UM, baada ya kutukia gharika ya janga la Vita Kuu ya Pili - mathalan, matokeo ya mazungumzo ya "Wajibu wa Kulinda Raia" yataisaidia jumuiya ya kimataifa kukabiliana vyema na masuala ya kuukinga umma dhidi ya mauaji ya halaiki, au kudhibiti matatizo yanayohusu jinai ya vita pamoja na uhalifu dhidi ya utu, na yatasaidia kukomesha vitendo vya utakaso wa mila za kijadi. Alisema "ni lazima tutathminie kidhati uwezo tulionao wa kimataifa, katika shughuli za kuokoa maisha ya umma ulio dhaifu ambao mara kwa mara hujikuta umenaswa kwenye mazingira yasio ya kawaida ndani ya mataifa yao." Aliahidi Pillay kwamba Ofisi ya Kamisheni juu ya Haki za Binadamu itaendelea kutekeleza majukumu iliodhaminiwa kimataifa, ya kutunza na kulinda kihakika haki za umma uliozingiwa na maafa yasio ya kawaida, kwa kuchukua hatua maalumu, za muda mrefu, za kuyakamilisha hayo. Alipendekeza kuanzishwe taasisi za kuhudumia shughuli hizo, na kuitaka UM kuhakikisha kunakuwepo ushirikiano wa kiufundi utakaoyasaidia pia yale makundi husika, kuhishimu haki za binadamu na kuzuia, vile vile, uharamishaji wa haki za binadamu.