Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

EU inashirikiana na FAO kupiga vita njaa kwenye nchi maskini

EU inashirikiana na FAO kupiga vita njaa kwenye nchi maskini

Ripoti za UM zimethibitisha ya kuwa katika 2009 watu bilioni moja ziada husumbuliwa na upungufu wa chakula na njaa sugu katika dunia.

Kwa hivyo, Mataifa ya Umoja wa Ulaya (EU) yameamua kuwasaidia wakulima wa nchi masikini, fungu ambalo limeathirika zaidi na mzoroto wa uchumi kwenye soko la kimataifa - ikichanganyika na athari haribifu za bei za juu za chakula - kupatiwa misaada ya yuro milioni 75, sawa na dola milioni 105, zitakazotumiwa kukuza uzalishaji bora wa kilimo kwenye maeneo yao. Msaada wa Umoja wa Ulaya utafadhiliwa nchi 13 katika maeneo ya Afrika, Asia, Karabiani na katika Amerika ya Kati, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO). Furushi la msaada wa fedha huo kutoka Umoja wa Ulaya (EU) linafuatilia mchango mwengine uliotolewa mwezi uliopita na EU, kufarajia nchi maskini, uliojumlisha yuro milioni 125 (dola milioni 170), msaada ambao UM ulichangishwa katika kipindi muhimu chenye kubainisha dhahiri mahitaji hakika yanayotakikana kuyavaua mataifa maskini na taathira haribifu za uchumi wa kimataifa ulizorota.