Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usubi waweza kufyekwa Afrika Magharibi kwa dawa ya 'ivermectin': WHO

Usubi waweza kufyekwa Afrika Magharibi kwa dawa ya 'ivermectin': WHO

Matokeo ya utafiti mpya wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kuhusu maradhi ya usubi (river blindness) katika sehemu za Afrika Magharibi, yamethibitisha kwamba ugonjwa huu unawezekana kukomeshwa kikamilifu na wataalamu wa kimataifa.

Uchunguzi wa WHO umeonyesha, kwa mfano, mataifa ya Mali na Senegal hayahitajii tena matibabu ya halaiki kudhibiti maradhi haya. Taarifa ya WHO ilieleza watu milioni 37, wameambukizwa na usubi, asilimia kubwa yao ikiwa watu masikini wenye kuishi kwenye jamii za vijijini barani Afrika.