Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA inasema inahitaji msaada wa bilioni $4.8 kukidhi mahitaji ya waathirika maafa ulimwenguni

OCHA inasema inahitaji msaada wa bilioni $4.8 kukidhi mahitaji ya waathirika maafa ulimwenguni

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti leo ya kuwa kuna upungufu wa dola bilioni 4.8 za msaada wa fedha zinazotakikana, katika miezi sita ya mwanzo wa 2009, kukidhi mahitaji ya kiutu kwa watu walioathirika na maafa.

Ofisi ya OCHA ilieleza ya kuwa tangu mwanzo wa mwaka, gharama za kuhudumia mahitaji ya jumla ya misaada ya kiutu, ikijumlisha maombi 16 ya jumla pamoja na maombi mawili ya dharura, yameongezeka kwa dola bilioni 1.5, na jumla hakika ya mchango unaohitajika kwa sasa hivi kuhudumia misaada ya dharura inakadiriwa dola bilioni 9.5.