Skip to main content

Makundi ya upinzani Usomali yateka nyara mali za UM

Makundi ya upinzani Usomali yateka nyara mali za UM

Majengo mawili ya UM katika Usomali ya Baidoa na Wajid yalishambuliwa hii leo na wapiganaji wapinzani wa kundi la Al Shabaab na walichukua vifaa na magari ya UM, kwa mujibu wa taarifa iliopokelewa kutoka Ofisi ya UM katika Usomali.

 Katika mji wa Baidoa, wizi wa zana za mawasiliano ya dharura na ukosefu wa maofisa wa usalama wa kimataifa, ni hali iliofunga UM kutoweza kutekeleza operesheni zake kama inavyohitajika kwenye eneo hili la mvutano. Ofisi ya UM katika Usomali inasema inasikitika kwamba imelazimika kuhamisha watumishi wake na kusimamisha, kwa muda operesheni zake katika Baidoa. Kuhusu mji wa Wajid, ambapo hali ya usalama, kwa wastani, bado haijabadilika UM umeripoti kuwa utaendeleza operesheni zake wakati ikitathminia namna ya kuimarisha huduma muhimu za kiutu kwa umma muhitaji wa Baidoa na raia waliopo kwenye sehemu nyengine za nchi katika Usomali.