Skip to main content

Misaada kwa utafiti wa chanjo ya ukimwi imeteremka

Misaada kwa utafiti wa chanjo ya ukimwi imeteremka

Ripoti mpya kuhusu uwekezaji, kwa mwaka 2008, kwenye utafiti wa kutafuta tiba kinga dhidi ya maambukizi ya VVU, mchango huo uliarifiwa kuteremka, kwa mara ya kwanza, tangu wataalamu walipoanza kukusanya takwimu juu ya utafiti wa chanjo kinga dhidi ya UKIMWI.

 Kwa mujibu wa ripoti, sababu kadha wa kadha ziliaminika kuwa chanzo cha mteremko - mathalan, mabadiliko kuhusu masuala ya kupewa umuhimu miongoni mwa wataalamu wa sayansi wa kimataifa yalisababisha mababdiliko hayo, au kuanguka kwa shughuli za kiuchumi, kwa ujumla, katika soko la kimataifa, au vile vile kutokana na ushindani miongoni mwa jumuiya za kisayansi kuhusu ajenda kuu ya afya inayofaa kupewa umuhimu. Lakini juu ya mteremko huu, mwelekeo wa uwekezaji kwenye miradi ya uchunguzi wa tiba kinga ya magonjwa uliongezeka tangu 2000. Michel Sidibé, Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Mashirika ya UM Dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) alinakiliwa akisema kwamba "utafiti unaohusu ile miradi ya kubuni vifaa vipya vya kujikinga na maambukizi ya maradhi ya UKIMWI ni muhimu sana katika kuzuia maambukizi mapya, na tafiti za kubuni chanjo kinga dhidi ya UKIMWI ndiyo huduma zenye matumaini imara ya kulikomseha janga hili milele, kimataifa."