Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO inasema itarekibisha utaratibu wa matangazo rasmi kuhusu A(H1N1)

WHO inasema itarekibisha utaratibu wa matangazo rasmi kuhusu A(H1N1)

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti leo kwamba ongezeko la kasi la idadi ya watu wenye kuambukizwa na maradhi ya homa ya mafua ya aina ya A(H1N1), katika nchi nyingi wanachama mnamo kipindi cha sasa hivi, ni tukio lenye kutatanisha juhudi za mataifa za kuthibitisha maambukizi ya maradhi kwa raia wao, kwa kulingana na vipimo vya kwenye maabara yao ya afya.

Kwa hivyo, WHO imearifu ya kuwa haitochapisha tena zile jedwali zenye kuonyesha takwimu zilizothibitisha idadi ya wagonjwa wa homa ya mafua ya H1N1 katika ulimwengu. Hata hivyo, WHO ilisema itakuwa inachapisha mara kwa mara, takwimu zitakazoelezea hali ilivyo kwenye mataifa yenye kuambukizwa, kwa mara ya kwanza na homa ya mafua ya H1N1, ikiwa miongoni mwa juhudi za kufafanua hali halisi ilivyo ya maambukizi ya magonjwa kimataifa. WHO itaendelea kuyaomba mataifa haya kuripoti uthibitishaji wao wa maambukizi ya kwanza ya homa ya mafua ya H1N1 na na kuchapisha idadi ya watu waathirika na udhibiti wa maradhi unavyoendelezwa katika ulimwengu.