Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchango wa NAM ni muhimu kwa suluhu ya kimataifa, asema KM

Mchango wa NAM ni muhimu kwa suluhu ya kimataifa, asema KM

KM Ban Ki-moon, ambaye hivi sasa yupo Misri, Ijumatano alihutubia Mkutano wa Hadhi ya Juu wa Jumuiya ya Mataifa Yasiofungamana na Madola Makuu (NAM), unaofanyika kwenye mji wa Sharm el-Sheikh.

Aliwaambia wajumbe wa Jumuiya ya NAM kwamba "mchango wao katika uhusiano wa kimataifa ni muhimu sana katika kusuluhisha mizozo ya dunia inayowakabili walimwengu kwenye mazingira ya sasa hivi." Alisema msimamo wa kundi la NAM, kuhusu ukuzaji wa huduma za maendeleo, na kwenye utekelezaji wa haki za kijamii ni maadili yenye kuchochea fukuto linalokaribishwa kihakika na mataifa wanachama wa UM, hususan kwenye mazingira ya ulimwengu uliofunikwa na matatizo ya uchumi dhaifu, unaoregarega, ikichanganyika na mizozo ya kifedha."