Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani ya chakula ndio msingi wa usalama wa dunia:IFAD

Amani ya chakula ndio msingi wa usalama wa dunia:IFAD

Kanayo Nwanze, Raisi wa Taasisi ya UM juu ya Mfuko wa Kimataifa kwa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kwenye mahojiano aliofanya na Redio ya UM alisisitiza juu ya umuhimu wa ile rai ya walimwengu kuhakikisha kunakuwepo akiba maridhawa ya chakula duniani.

Alisema kadhia hii ndio msingi wa kuimarisha usalama wa ulimwengu. Kadhalika Nwanze alisema wakati umewadia kwa nchi wanachama kupunguza msisitizo wa kufadhilia misaada ya chakula kwa umma muhitaji, na badala yake alipendekeza kufanyike uwekezaji wa muda mrefu kwenye huduma za uzalishji wa kilimo katika mataifa yanayoendelea.